Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la AhlulBayt (a.s) -ABNA-, sambamba na siku za maombolezo ya Shahidi Bibi Fatima Zahra (a.s), wanafunzi wa Chuo cha Dini cha Kiislamu cha Nigeria waliandaa hafla ya maombolezo huko katika mji mtukufu wa Karbala. Katika hafla hiyo, wanafunzi hao walitoa heshima zao kwa binti wa Mtume Mtukufu (s.a.w.w) kupitia kaswida, hotuba na dua, huku wakikumbuka nafasi ya juu ya Bibi Zahra (a.s) katika historia ya Uislamu na kujitolea kwake katika kulinda Uislamu na haki. Tukio hilo lilihudhuriwa pia na baadhi ya masheikh, wanafunzi wa vyuo vya dini kutoka nchi nyingine, na wageni waliokuwa wakifanya ziara katika Haram takatifu ya Imam Hussein (a.s).

9 Novemba 2025 - 15:20

Habari Pichani | Marasimu ya Maombolezo ya Wanafunzi wa Chuo cha Dini cha Nigeria huko Karbala

Your Comment

You are replying to: .
captcha